Entrance Form -F1 – 2025/2026
Tafadhali pakua form na jaza taarifa sahihi na rudisha fomu ofisi ya usajili shule ya Sekondari Loyola Jengo la Utawala, chumba Na. A009. Mtihani wa kwanza wa Usahili (first interview) utafanyika siku ya Ijumaa, 19 Septemba 2025 saa 1:00 asubuhi na mwisho wa kurudisha Fomu ni siku ya Alhamisi, 18 Septemba 2025 saa Tisa Alasiri.
Mtihani wa Pili wa Usahili (second interview) utafanyika siku ya Ijumaa, 26 Septemba 2025 saa 1:00 asubuhi na mwisho wa kurudisha Fomu ni siku ya Alhamisi, 25 Septemba 2025 saa Tisa Alasiri.
Mtihani wa kujiunga na kidato cha kwanza kwa Dar es Salaam na mkoani utafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 27 Septemba 2025 saa mbili asubuhi. Mzazi/ mlezi unaombwa kurudisha fomu katika kituo atakachofanyia mtihani mwanafunzi. Vituo vya mtihani ni kama ifuatavyo:
Ø Mwanza – Mtihani wa usaili utafanyikia Parokia ya Nyakahoja
Ø Dodoma – Mtihani wa usaili utafanyikia Shule ya msingi ya Mt. Inyasi
Ø Arusha na Moshi – Mtihani wa usaili utafanyikia Notre Dame shuleni Temdo, Njiro
Mwanafunzi anapaswa kurudisha fomu hii ikiambatana na vitu vifuatavyo:
1. (a) Nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mwanafunzi au Hati ya kiapo cha mahakama inayothibitisha tarehe ya Kuzaliwa na jina kamili la mwanafunzi.
2. (b) Mwanafunzi anapaswa kuwa amehitimu darasa la saba kabla ya 31 Disemba 2025. Mwanafunzi wa darasa la sita hastahili.
(c) Picha mbili ndogo (Passport size) za mwanafunzi ambazo amepiga hivi karibuni.
(d) Risiti ya malipo ya fomu. (fomu haitapokelewa bila risiti ya malipo)
3. Sehemu ‘B’ ya fomu hii inapaswa kujazwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi aliyosoma mwanafunzi.
4. Gharama ya fomu ni Tshs. 25,000/=, mara baada ya kununua fomu pesa HAITARUDISHWA.