NAFASI ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2025
Uongozi wa shule ya Sekondari Loyola inayomilikiwa na Mapadre wa Shirika la Yesu (Majesuit) unapenda kuwatangazia wazazi/walezi na wanafunzi nafasi za kujiunga na masomo Kidato cha Kwanza 2025. Shule inapo-kea wanafunzi wa madhehebu na jinsi zote. Shule ni ya Bweni kwa wasichana na kutwa kwa wavulana.
Fomu za kujiunga zinapatikana katika shule ya Sekondari ya Loyola, Msimabazi Centre: chumba namba 19, Chumba namba 22, Parokia ya K/Ndege Dodoma, Parokia ya Nyakahoja Mwanza, Notre Dame Schools, Temdo, Njiro na katika tovuti ya Shule www.loyola.ac.tz. Pia nafasi za kujiunga na kidato cha Tano 2024/2025 na nafasi za kuhamia kidato cha Pili na kidato cha tatu 2025 Fomu zinapatikana Shuleni na kwenye Tovuti ya shule tu.
GHARAMA ZA FOMU
- Kidato cha Kwanza TShs. 25,000/=
- Kidato cha Pili TShs. 30,000/=
- Kidato cha Tatu TShs. 30,000/=
- Kidato cha Tano TShs. 25,000/=
Malipo ya fomu yafanyike kwenye Akaunti ya shule; tawi la CRDB Akaunti Namba 0150315988101 Jina la Akaunti: LOYOLA HIGH SCHOOL. Karatasi ya malipo (bank pay-in-slip) iambatanishwe na fomu ya kujiunga kwa uthibitisho zaidi. Au LIPA NAMBA 5132307 LOYOLA HIGH SCHOOL. Fomu haitapokelewa bila risiti (bank pay-in-slip) ya malipo.
TAREHE ZA USAILI – DAR ES SALAAM SHULE YA SEKONDARI LOYOLA
- Kidato cha I
- Mtihani wa usaili wa kwanza Ijumaa tarehe 20 Septemba 2024.
- Mtihani wa usaili wa pili Jumamosi tarehe 28 Septemba 2024.
- Kidato cha Pili na Tatu
- Mtihani wa usaili wa tatu Jumatano tarehe 11 Desemba 2024.
MIKOANI: KIDATO CHA KWANZA TU, USAILI UTAFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 28 Septemba 2024 TU
- Mwanza mtihani wa usaili utafanyika Parokia ya Nyakahoja.
- Dodoma mtihani wa usaili utafanyika shule ya Msingi Mt. Inyasi.
- Arusha na Moshi mtihani utafanyika Notre Dame Schools, Temdo, Njiro.
MUDA WA KAZI
Kuanzia Saa mbili kamili Asubuhi hadi saa tisa kamili Alasiri siku za Jumatatu mpaka Ijumaa.
MAHALI ILIPO SHULE
Shule ya Loyola iko eneo la Mabibo Farasi, kama kilometa 10 Magharibi mwa Jiji la Dar es Salaam. Shule iko katikati ya barabara kuu mbili Mandela na Morogoro. Lango kuu la shule liko katika Barabara ya Kigogo. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi muda wa kazi simu namba: 0769-844812, 0785-805115, 0658-233088.